Grace Mugabe astakiwa kwa kumshambulia mwana mitindo, Afrika Kusini

Serikali ya Zimbabwe inatafuta kinga ya kidiplomasia kwa mkewe rais Robert Mugabe katika kesi moja dhidi yake ambapo anadaiwa kumshambulia mwana mitindo mmoja nchini Afrika kusini kwa mujibu wa wizara ya maswala ya polisi nchini Afrika kusini. Grace Mugabe yungali nchini Afrika kusini licha ya habari kuwa alikuwa amerejea nchini Zimbabwe.A� Mwanamitindo mmoja mwenye umri wa miaka 20 kutoka afrika kusini amemshtumu Bi Mugabe kwa kumshambulia katika hoteli moja jijiniA� Johannesburg siku ya jumapili.A� Polisi walitarajia biA� Mugabe mwenye umri wa miakaA� 52 kufika mahakamani lakini hakufika.