Gor Mahia kuwania kufuzu kwa raundi ijayo ya kilabu bingwa Barani Afrika

Mabingwa wa ligi kuu ya soka humu nchini Gor Mahia, watawania kufuzu kwa raundi ijayo ya ligi ya kilabu bingwa Barani Afrika itakapomenyana naA�A�na Leones Vegeteranios ya Equatorial GuineaA�A�kwenye mechi ya marudiano jijini Malabo leo saa moja usikumsaa za Afrika Mashariki.

KOa��gallo ina nafasi nzuri ya kufuzu baada ya kushinda mechi ya mkondo wa kwanza mabao mawili kwa bila mjini Machakos,A�A�juma lililopita. Timu hiyo inayofunzwa na Dylen Kerr,A�A�ilifanya mazoezi ya kwanza jana jioni jijiniA�A�Malabo,A�A�baada ya kuondoka humu nchini Jumatatu iliyopita.

Wakati uo huo,A�AFC Leopards pia iko ugenini jijini Mahajanga, Madagaska itakakochuana na wenyeji FOSA Juniors adhuhuri hii, katika mechi ya mkondo wa pili wa kombe la mashirikisho Barani Afrika. Ingwe inahitaji ushindi wa mabao mawili kwa bila, kwenye mechi hiyo ili ifuzu kwa mechi ya raundi ya kwanza baada ya kutoka sare bao moja kwa moja katika mechi ya mkondo wa kwanza iliyochezwa juma lililopita, mjini Kakamega. Kikosi cha a�?Ingwea�� kitakosaA�huduma za mshambulizi Mnaijeria, Henry Uche aliyejeruhiwa.