Gor Mahia kuchuana na Leones Vegeteranios ya Equatorial Guinea

Mabingwa wa ligi kuu ya Sportpesa Gor Mahia, watachuana na Leones Vegeteranios ya Equatorial Guinea, katika raundi ya kwanza ya kipute cha kuwania kombe la kilabu bingwa Barani Afrika.Gor Mahia itanuia kufanya vyema Barani Afrika baada ya kuridhisha zaidi humu nchini na kutwaa ubingwa wa ligi mwaka huu kwa mara ya 16. Mshindi wa mechi hiyo atacheza na mshindi wa mchuano baina ya Esperance ya Tunisia na Asac Concorde ya Mauritania. Katika mechi za kuwania kombe la mashirikisho, AFC Leopards ya Kenya itachuana na Fosa Juniors ya Madagaska huku mshindi akimenyana na mshindi wa mechi baina ya Ngazi Sports ya visiwa vya Ngazija na ASPL 2000 ya Mauritius. Mechi hizo zitachezwa mwezi Februari mwaka ujao.

Wakati uo huo, madereva ishirini na sita wamesajiliwa kushiriki katika makala ya nne ya mashindano ya mbio za magari ya a�?Champagnea�? yaliyozinduliwa jana jijini Nairobi na yatakayandaliwa Jumamosi hii katika kaunti ya Kajiado. Madereva watakinzana katika vitengo vitatu; kitengo cha wanaoanza, waliozoea na wenye umahiri mkubwa. Mbio hizo zitakuwa za umbali wa takriban kilomita kumi zenye sehemu nane zenye ushindani mkali. Washiriki katika kitengo cha wanaoanza mashindano hayo ni shilingi 3,500, wale wa kitengo cha waliozoea watalipa shilingi 5,500 na madereva waliobobea, watalipa ada ya shilingi 7,500. Washindi katika kila kitengo watatuzwa nishani na vikombe.