Gladys Wanga apinga hatua ya SRC kupunguza mishahara ya wambuge

Mwakilishi wa wanawake kaunti ya Homabay Gladys Wanga sasa anadai kuwa hatua ya tume ya mishahara ya kupunguza mishahara ya wabunge haikuwa na niya njema,akidai tume hiyo haikufanya utafiti kabla ya kuchapisha mishahara mipya ya wabunge. Wanga aliongeza kwamba kuna njama ya kuwadunisha wabunge lakini akakariri kwamba hakuna mbunge anayetetea kuongezwa mshahara huku akikariri kwamba mishahara iliyoko haifa kupunguzwa. Wanga ambaye ni mwanachama wa tume ya kuwaajiri wahudumu wa bunge alisema kuwa tume ya mishahara na marupurupu, SRC,A� haikutathmini kazi zao kabla ya kuchapisha kwenye gazeti rasmi la serikali viwango vipya vya mishahara akiongeza kusema kuwa hawatatazama tu huku tume hiyo ikifedhehesha bunge. Alikariri kwamba wabunge hawaitishi nyongeza ya mishahara ila wameridhika na ile wanayoipata. Wanga alisema kuwa ni makosa kwa tume ya SRC kupunguza mikopo ya wabunge ya ununuzi wa nyumba na kuingilia ruzuku ya ununuzi wa gari akisema mawaziri na makatibu wa wizara wananufaika pia kutokana na pesa hizo.