Gitobu Imanyara akihama chama cha ODM

Aliyekuwa mbunge wa A�Imenti ya kati Gitobu Imanyara, amekihama chama cha ODM na kujiunga na chama cha Maendelo Chap Chap, atakachogombea kiti cha ubunge cha Imenti ya Kati. Wakili huyo alifanya maamuzi hayo baada ya kufanya mkutano wa faragha na viongozi wa eneo hilo . A�Imanyara alikua ametangaza kuwa atajiuzulu kutoka kwa siasa kakamavu baada ya kushindwa katika kinyanga��anyiro cha useneta katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2013. Aliwania kiti hicho kwa tiketi ya chama cha ODM , na kupata kura 48,050 dhidi ya Kiraitu Murungi aliyepata kura A�361,897. Wengine wanaowania kiti hicho cha ubunge ni pamoja na mbunge wa sasa Gideon Mwiti A�na katibu wa kaunti ya Meru Gideon Kimathi.