Githu Muigai awasilisha kesi kupinga uhalali wa bunge la mwananchi

Mwanasheria mkuu Githu Muigai amewasilisha kesi katika mahakama ya Milimani chini ya hatua ya dharura kupinga uhalali wa kikatiba wa bunge la wananchi linalobuniwa katika mabunge 15 ya kaunti nchini. Katika taarifa yake ya kiapo iliyowasilishwa na naibu wa wakili mkuu wa serikali Charles Mutinda, mwanasheria mkuu anataka kesi hiyo isikizwe kutokana na umuhimu wake kutokana na sababu kwamba kuna ukiukaji wa katiba unaoendelea na matumizi ya rasilmali za umma kwa shughuli zisizokuwa halali kupitia kubuniwa kwa mabunge ya wananchi. Alisema kwamba swala hilo linapaswa kuchukuliwa kuwa la dharura ili rasilmali za umma zisizendelea kutumika kwa shughuli zisizokuwa halali kikatiba na sheria ya usimamizi wa fedha za umma. Pia alisema kwamba swala hilo linaibua maswali muhimu ya kisheria yaliyo na umuhimu kwa umma.A�A�Kaunti za Mombasa, Kwale, Kilifi, Mandera, Kitui, Machakos, Makueni, Kakamega, Vihiga, Bungoma, Busia, Siaya, Kisumu, Homa Bay na Migori zimepitisha hoja ya kubuniwa kwa mabunge ya wananchi