Giorgio Chiellin huenda asicheze mechi ya ufunguzi ya ligi dhidi ya Barcelona

Mlinzi wa Juventus Giorgio Chiellini huenda asicheze mechi ya ufunguzi ya ligi ya kuwania kombe la kilabu bingwa barani Ulaya dhidi ya Barcelona kwasababu ya jeraha. Chiellini aliumia katika kambi ya mazoezi ya timu ya taifa ya Italia siku ya Ijumaa na kukosa kushiriki mechi za kuwania kombe la dunia dhidi ya Uhispania na Israel. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 33 amerejea jijini Turin licha ya Juventus kusema kuwa atapona kwa haraka. Chiellini huenda asicheze mechi ya ligi kuu ya a�?Serie-Aa�� dhidi ya Chievo tarehe 9 mwezi huu na pia mechi ya bara Ulaya dhidi ya Barcelona uwanjani Camp Nou siku tatu baadaye. Mabingwa hao mara mbili wa bara Ulaya walishindwa katika fainali ya mwaka huu mabao 4-1 na Real Madrid jijini Cardiff mwezi Juni.