Gideon Moi amehimizi serikali kushughulikia ukosefu wa usalama Baringo

Seneta wa kaunti ya Baringo, Gideon Moi, amehimiza serikali kushughulikia kikamilifu suala la ukosefu wa usalama katika kaunti ya Baringo inayokumbwa na zogo. Akiwahutubia waalimu wa kaunti ya Baringo wakati wa mkutano ulioandaliwa jana, seneta huyo wa Baringo alisema ni jukumu la serikali kuhakikisha usalama wa raia wake. Alisema sekta ya elimu katika kaunti hiyo pia imeathiriwa na visa vya utovu wa usalama kwani imewapoteza waalimu wawili na baadhi ya shule kufungwa.Wakati huo huo viongozi wa upinzani wakiongozwa na Raila Odinga pia wamemhimiza mwenyekiti wa kamati ya usalama wa taifa katika bunge la taifa Asaman Kamama ambaye pia ni mbunge wa Tiaty kujiuzulu kwa minajili ya kupatikana amani katika eneo hilo. Alisema watu wenye mkinzano wa maslahi hawapaswi kuruhusiwa kusimamia mikakati ya kutafuta amani katika eneo hilo.