Gideon Malyungi amtetea Ngilu kwa kupiga marufuku uchomaji wa makaa Kitui

Mbunge wa Mwingi ya kati, Gideon Mulyungi, amemtetea gavana wa Kitui, Charity Ngilu, kwa kupiga A�marufuku uchomaji na usafirishaji haramu wa makaa huko Kitui, hatua ambao imezua malalamishi kutoka wafanyibiashara katika kaunti jirani, baada ya lori lililokuwa likisafirisha makaa hadi kaunti ya Kiambu kuteketezwa. Mulyungi alisema hatua hiyo ya gavana haipswi kuchukuliwa kwamba inalenga jamii yoyote huko Kitui bali ni mapambano dhidi ya uharibifu wa mazingira ambayo yapasa kuungwa mkono na kila mkazi wa kaunti ya Kitui.