Ghasia yazuka Afrika Kusini baada ya wakulima wawili wazungu kuachiliwa

Ghasia zimekumba mji mmoja mdogo nchini Afrika kusini baada ya hakimu mmoja kuwachilia kwa dhamana wakulima wawili wazungu ambao wanashtakiwa kwa kumuua kijana mmoja mwafirika mwenye umri wa miaka 16. Gadhabu ilitanda katika mji huo unaofahamika kwa uzalishaji wa mahindi waA� Coligny baada ya wakazi kugundua kuwa washukiwa hao wawili walikuwa wameachiliwa huru. Nyumba tatu ziliteketezwa huku maduka ya wazungu yakiporwa.A� Ghasia hizo zinaashiria kukithiri kwa taharuki ya ubaguzi wa rangi katika baadhi ya maeneo nchini humo. Tatizo la ubaguzi wa rangi lilishuhudiwa nchini Afrika kusini hadi mwaka waA� 1994 ambapo taifa hilo lilifanya uchaguzi wake wa kwanza wa kidemokrasia.A� Vyombo vya habari nchini humo vilisema kuwa wakulima hao wawili wazungu walimpata kijana huyo akiiba maua katika shamba moja mjini humo wakamkamata na kumpiga. Hata hivyo wanadai kuwa mvulana huyo aliruka kutoka kwa lori walipokuwa wakimpeleka katika kituo cha polisi.