Ghasia Ufaransa Dhidi Ya Wabomozi Vibanda

Kulitokea vurugu wakati kundi la wabomozi lilipoanzisha shughuli ya kubomoa mabanda ya wakimbizi katika mji wa bandari wa Calais,nchini Ufaransa.Polisi wa kutuliza fujo walikabiliwa na wakimbizi hao walipokuwa wakibomoa mabanda hayo,huku 12 yakiteketezwa.Wabomozi hao walilenga mabanda yaliokuwa tayari yana watu,kusini mwa mji huo.Serikali hiyo ina mipango ya kuwapeleka wahamiaji kwenye kambi maalum za kuwapokea wakimbizi.Wahamiaji hao,ambao wengi wao ni raia wan chi za mashariki ya kati,Afghanistan na bara Afrika,wanatarajia kuvuka na kuingia barani ulaya kwa njia isio halali.