George Magoha aitisha mkutano wa waziri wa afya kushughulikia changamoto zinazokumba KNH

A�Mwenyekiti wa bodi ya madaktari na wataalam wa meno A�nchini Prof. George Magoha,A�A�ameitisha mkutano na waziri wa afya Sicily Kariuki,ili kushughulikia kwa dharura changamoto zinazokumba hospitali kuu ya Kenyatta.Alisema mkutano huo ambao umepangiwa kufanyika leo pia utashughulikia tofauti zilizoko baina ya madaktari wanaopokea mafunzo ya maalum na wasimamizi wa hospitali hiyo kwa lengo la kurejesha huduma za kawaida katika taasisi hiyo haraka iwezekanavyo. A�A�Madaktari hao 700 wanaopokea mafunzo ya kuwa wataalam wa kimataibabu walianza mgomo wao kufuatia kusimamishwa kwa wenzao kutokana na kisa ambacho mgonjwa mmoja alifanyiwa upasuaji wa kichwa ambao hakuhitaji katika hospitali hiyo.Bodi hiyo inaruhusiwa chini ya sheria za nchi hii kuthibiti shughuli za madaktari,wataalam wa meno na taasisi za kimatibabu nchini.