George Bush aruhusiwa kutoka hospitalini

Aliyekuwa rais wa Marekani George H.W.Bush ameondoka hospitali moja mjini Texas,ambako alikuwa amelazwa kwenye chumba cha wagonjwa mahututi kufwatia ugonjwa wa kichomi.Mwanasiasa huyo mwenye umri wa miaka 92 alilazwa katika hospitali ya kiMethodist ya Houston tarehe 14 mwezi wa Februari.Aidha mke wake Barbara Bush ,mwenye umri wa miaka 91A� alilazwa kwa muda mfupi kwenye hospitali hiyo na kutibiwa kwa mavune na kikohozi.George Walker Bush,ambaye alikuwa rais waA� 41 wa Marekani alihamishwa hadi sadaruki ya hospitali hiyo ambako madaktari walimtibu kwa kutumia mipira ya kumsaidia kupumua na hatimayeA� kumruhusu kwenda nyumbani.Bush alihudumu kama rais wa MarekaniA� kati ya miaka ya 1989-1993.Kiongozi huyo pia aliwahi kulazwaA� katika hospitali ya Maine mnamo mwaka wa 2015 baada ya kuvunjika mfupa wa shingoni.Aidha kiongozi huyo anaugua kutokana na ugonjwa wa kutetemeka mikono na kwa sasa anatumia kitimaguru.Alizaliwa mwaka wa 1924 mjini Massachussets na amewahi kuhudumu kama mbunge na mkurugenzi wa shirika la ujasusi la CIA na pia kuwa makamu wa rais Ronald Reagan.Mwanawe,George Bush alichaguliwa kuwa rais mnamo mwaka 2000 na kuhudumu vipindi viwili akiwa rais wa 43 wa Marekani.