Gavana Wa Taita Taveta Aitaka Serikali Kuu Kuwajibika

Gavana wa kaunti ya Taita Taveta John Mruttu ametoa wito kwa serikali ya kitaifa kuharakisha hatua ya kuhamisha na ujenzi wa barabara katika maeneo ya kaunti . Mruttu amesema uchukuzi, barabara, ujenziA� na ukarabati wa barabara , reli na majengo , ndege, nyumba na mawasiliano zinafaa kupewa kipaumbele. A�Mruttu alikuwa akiongea katika hoteli moja jijini A�Nairobi wakati wa kongamano la wadau kuhusu barabara lililoandaliwa na kamati ya seneti kuhusu barabara na uchukuzi inayoangazia sekta ya barabara. A�Aidha amesema mswada wa mwaka 2015 A�kuhusu barabara humu nchini utatekeleza wajibu muhimu katika kusimamia wakati wa ujenzi wa barabara uorodheshaji. Naibu spika wa seneti Kembi Getura amesema malengo ya kongamano hilo ni kubuni mpango wa kuhamishwa kwa majukumu ya barabara na kuchunguza mswada wa mwaka 2015 wa barabara za humu nchini.