Gavana wa Nyeri kuzikwa wiki ijayo

  • Marehemu Gavana wa kaunti ya Nyeri aliyefariki jana katika ajali ya barabarani Dr. Wahome Gakuru atazikwa siku ya jumamosi juma lijalo katika eneo la Kirichu mjini Nyeri. Mipango ya mazishi imeanza katika kaunti yake ikiongozwa na aliyekuwa naibu wake A�Mutahi Kahiga. A�Kahiga alisema kuwa walichagua tarehe hiyo ili kumwezesha mwanawe wa kiume ambaye anafanya mtihani wa kitaifa wa kidato cha nne KCSE kuhudhuria mazishi hayo. Kahiga aliepuka kutoswa katika swala la urithi huku akisema kuwa uongozi wa kaunti hiyo umejitolea kumsindikiza Dr. Gakuru kwa njia inayostahili. Aliwahakikishia wakazi kuwa hakutakuwa na pengo la uongozi kwa vile wamejitolea kuhakikisha kuwa wanatimiza kikamilifu maono ya marehemu gavana huyo. A�Alimtaja Gakuru kuwa kiongozi mwenye maono huku akiongeza kuwa kifo chake kilikuwa pigo kubwa kwa wakazi wa eneo hilo ambao walimpigia kura kwa wingi wakati wa ucahguzi mkuu uliopita wakiwa na matarajio makubwa ya kupata huduma bora.

A�