Wakazi wa Baringo wataka serikali kuimarisha usalama

Wakazi wa kaunti ya Baringo wanaoishi katika maeneo yanayokumbwa mara kwa mara na visa vya utovu wa usalama wamehimiza serikali ya kaunti hiyo kutekeleza operesheni kali ya usalama katika maeneo hatari zaidi kwenye kaunti hiyo. Wakazi hao wamesema majambazi wanavuruga amani usiku na mchana licha ya kuwepo kwa maafisa wa usalama katika eneo hilo. Hii ni baada ya msururu wa mashambulizi yaliyosababisha vifo vya watu wawili na huku mifugo kadhaa wakiibwa. washukiwa wa ujambazi kutoka jamii ya Wa-Pokot katika muda wa siku chache zilizopita. Mwanachama maalum wa bunge la kaunti hiyo, Meja Kimunyan amesema majambazi wanaendelea kuwakosesha usingizi wakazi wa kaunti hiyo licha ya serikali kuwapeleka maafisa wa jeshi la KDF kukabiliana na wahalifu hao. Kimunyan amesema wakazi wanahofia maisha yao kwani majangili hao hawajanaswa.A�Joshua Korir, ambaye ni mmoja wa waathiriwa waliofurushwa na majambazi kutoka makaazi yao na sasa anaishi kambini huko Moinonin pamoja na waathiriwa wengine elfu mbili amesema serikali imewatelekeza.