Gavana wa Kitui Charity Ngilu ampigia debe Raila Ukambani

Huku siasa za Ukambani zikiendelea kupamba moto kabla ya marudio ya uchaguzi wa urais gavana wa Kitui Charity Ngilu amesema atawahimiza viongozi wa Ukambani wanaoegema mrengo wa NASA kuhakikisha wakazi wa eneo hilo wanampigia kura mwaniaji urais wa upinzani Raila Odinga na mwaniaji wake mwenza Kalonzo Musyoka. Ngilu alikuwa akihutubu kwenye mkutano mjini Kitui wa wabunge na wanachama wa baraza la kaunti ya Kitui. Viongozi hao akiwamo mbunge wa Kitui ya kati Makali Mulu na mwenzake wa Mwingi ya kati Gideon Mulyungi, pia walishtumu matamshi yanayotolewa na baadhi ya viongozi wa Jubillee dhidi ya majaji wa mahakama ya juu.