Gavana wa Kiambu Ferdinard Waititu kuajiri wauguzi wa muda

Gavana wa kaunti ya Kiambu, Ferdinand Waititu amesema serikali ya kaunti hiyo itaajiri wauguzi wa muda ili kuwaondolea masaibu wakazi wa kaunti hiyo ambao hawawezi kugharamia huduma za matibabu katika hospitali za binafsi. Waititu amesema hatua hiyo itatekelezwa huku wakiendelea kushauriana na wauguzi wanaogoma kuwashawishi kurejeaa kazini. Akiongea alipozuru hospitali ya Kiambu Level 4, Waititu aliwahakikishia wakazi kuwa huduma za matibabu katika hospitali za umma zitarejea siku kadhaa zijazo na kwamba atakutana na viongozi wa eneo hilo kutafuta suluhu kwa changamoto zinazokumba sekta ya afya katika kaunti hiyo.