Gavana Tunai ahimiza jamii ya Wa-Maasai kumpigia kura rais Kenyatta

Gavana wa Narok, Samuel Tunai amehimiza jamii ya Wa-Maasai kumpigia kura rais Uhuru Kenyatta kwenye uchaguzi mkuu wa mwezi agosti akisema hana imani na upinzani ambao lengo lake kuu ni kujitafutia kura bila kujali maslahi ya jamii hiyo. Tunai amesema serikali ya Jubilee ndiyo itashughulikia mahitaji ya jamii ya Wa-Maasai. Kwingineko,A�mbunge waA�A�Bahati, Kimani Ngunjiri amewataka wanasiasa wajiepushe na kampeni ambazo zitachocheaA�rabusha. Naye mgombea urais wa mrengo wa NASA, Raila Odinga amesitisha kampeni zake kwa muda huku wafuasi wake wakitafakari iwapo atashiriki katika mjadala wa urais utakaoandaliwa leo katika chuo kikuu cha kikatoliki cha Afrika Mashariki.