Gavana Ojaamong Azuru Zahanati

ojaamong

Gavana wa kaunti ya Busia, Sospeter Ojaamong aliwashangaza maafisa wa matibabu kwenye zahanati ya Amaase katika eneo la Teso Kusini alipoingia katika famasi ya zahanati hiyo na kuanza kukagua dawa.

Ojaamong pia alizuru kitengo cha wgonjwa wanaotibiwa na kurudi nyumbani ambapo alifahamishwa kuwa kuna dawa za kutosha. Ziara yake ilifuatia madai ya baadhi ya viongozikuwa vituo vya afya katika kaunti hiyo havina dawa.

Ojaamong alisema kuna dawa za kutosha katika kituo cha kuhifadhia dawa huko Matayos na kushangaa ni kwanini watu wanaeneza uvumi. Aidha Ojaamong alizuru vituo vya afya vya Changara na Osieko ambako wakazi walithibitisha kwamba kuna dawa za kutosha. Serikali ya kaunti ya Busia imeongeza fedha za ununuzi wa dawa kutoka shilingi milioni-150 hadi milioni-350. Alisema chuo cha mafunzo ya utatibu huko Busia kitachukua kundi la kwanza la wanafunzi mwezi ujao na kuwashauri wazazi kujitokeza kuchukua fomu za kujaza.