Ojaamong Atarajia mgomo wa madaktari utaisha

Habari nyingine zasema, gavana wa kaunti ya Busia, Sospeter Ojaamong ameelezea matumaini yake kuwa mazungumzo yanayoongozwa na katibu mkuu wa COTU, Francis Atwoli yatakomesha mgomo wa madaktari uliodumu kwa zaidi ya miezi miwili hapa nchini. Gavana huyo alisema Atwoli amejitolea kuafikia suluhisho kwa mzozo huo kupitia mashauriano. Hata hivyo aliwahimiza madaktari kulegeza msimamo wao na badala yake kushiriki kwenye mazungumzo hayo ili kuwaondolea dhiki wagonjwa ambao hawawezi kupata matibabu maalum kwenye hospitali za umma.A�OjaamongA� alisema mkataba wa mwaka 2013 una dosari kwani haukutiwa saini na waziri wa afya wakati huo na pia hautambui serikali za kaunti. Alisema mfumo wa sasa unawapa madaktari uwezo mkubwa, jambo ambalo limeathiri sekta ya afya hapa nchini. Alitoa mfano wa kaunti ya Busia ambapo alisema kati ya madaktari 35 walio katika kaunti hiyo, 17 wako kwenye likizo ya masomo ya kati ya miaka minne na mitano ilhali wanaendelea kupokea mshahara bila kutoa huduma zozote.