Gavana mteule Ferdinand Waititu aahidi kutekeleza ahadi alizotoa

Gavana mteule wa kaunti ya Kiambu Ferdinand Waititu ameahidi kufanya kazi bega kwa bega na kundi lake ili kuwapa wakazi wa kaunti hiyo ahadi alizotoa wakati wa kampeini za uchaguzi. Waititu aliahidi kukabiliana na pombe haramu ambayo imewaathiri vijana wengi katika kaunti hiyo. Pia aliwaonya maafisa wanaoshirikiana na walanguzi wa dawa za kulevya akisema serikali ya kaunti yake itashirikiana na serikali ya kitaifa katika kukabiliana na biashara hiyo haramu. Matamshi yake yaliungwa mkono na naibu wake James Nyoro ambao aliwahakikishia wakazi wa kaunti hiyo kwamba watashirikiana kikazi. Mbunge mteule wa kaunti ya KiambuA� Gathoni Muchomba pia alikuwepo.