Gavana Kidero, Ruto, na Kabogo hatarini

Kinyanga��ayiro kikali bado kinashuhudiwa kati ya wawaniaji wawili muhimu wa kiti cha Ugavana cha Kaunti ya Nairobi. Mike Mbuvi Sonko ambaye anaongoza kwa kura 642,741 dhidi ya Gavana wa sasa Evans Kidero ambaye amepata kura 513,556.A�A� Katika Kaunti ya Bomet, Joyce Laboso wa chama cha Jubilee amechukua uongozi wa mapema kwa kupata kura 156,989. Gavanma wa sasa Isaac Ruto wa Chama Cha Mashinani amepata kura 74,781.

Katika Kaunti ya Kiambu, muwaniaji wa chama cha Jubilee, Ferdinand Waititu, anaongoza kwa kura 661,488, ilhali Gavana wa sasa William Kabogo amepata kura 176,493.

Katika Kaunti ya Kakamega Gavana wa sasa Wyclife Oparanya wa chama cha ODM anaongoza kwa kura 214 472 ilhali mpinzani wake wa karibu ambaye ni seneta wa Kakamega, Bonny Khalwale wa chama cha Ford-Kenya amepata kura 82,085.

Katika Kaunti ya Kajiado,muwaniaji wa chama cha Jubilee Joseph Ole Lenku anaongoza kwa kura 118,208 akifuatiwa na Gavana wa sasa David Nkedianye wa chama cha ODM ambaye amepata kura 99,738.