Gavana Kabogo Aahidi Kuajiri Madaktari Kutoka India

Huku mgomo wa madaktari ukiendelea, gavana wa kaunti ya Kiambu William Kabogo amesema serikali ya kaunti hiyo itaajiri madaktari kutoka India kupiga jeki huduma zinazotolewa na wauguzi kwenye kaunti hiyo. Kabogo amesema kuwa serikali hiyo iko katika harakati za kuajiri madaktari watakaoafiki masharti ya kazi yalioratibiwa na serikali ya kaunti hiyo. Akiongea na wahudumu wa afya kwenye kaunti hiyo, Kabogo alidai kuwa madaktari wanaogoma hawana utu na hawajali kabsa baada ya kukataa asilimia 40 ya nyongeza ya mshahara iliyopendekezwa na serikali akisema hiyo niA� ishara kuwa hawadhamini maisha ya binadamu. Kabogo alisifia kazi ya wahudumu wa afya wanaojitolea katika jamii akisema wamesaidia kupunguza gharama ya utoaji matibabu katika vituo vya afya. Waziri wa afya kaunti ya Kiambu, Jonah Mwangi alisema mipango inafanywa kuratibu sheria ya kuwapa marupurupu wahudumu hao wa afya ili kuwamotisha.