Gavana Javier Duarte arejea nyumbani baada ya kutimuliwa Guatemala

Aliyekuwa Gavana wa Jimbo la VeracruzA� mashariki mwa Mexico amerejea nyumbani baada ya kutimuliwa nchini Guatemala. Javier Duarte alikuwa ametuhumiwa kwa ufisadi, ulanguizi wa fedha na kujihusisha naA� makenge ya uhalifu wa kupanga. Duarte alijiuzulu wadhifa wake mwezi Oktoba mwaka 2016 na hatimaye kutoweka hadi alipokamatwa miezi sita baadaye katika hoteli moja huko Guatemala. Duarte alizuiliwa katika mji wa Solola kufuatia operesheni ya pamoja kati ya shirika la polisi la kimataifa a�?Interpola�? na maafisa wa polisi nchini Guatemala. Anashukiwa kwa kuiba dolla milioni-35 za Marekani (pesa za Umma) ambazo ziliekezwa katika msururu wa kampuni za mafuta. Kulikuwa na msururu wa visa vya ghasia na ufisadi katika Jimbo la VeracruzA� wakati wa utawala wake wa miaka sita.