Gavana Hussein Doda atetea maendeleo yaliyopatikana chini ya uongozi wake

Gavana wa Kaunti ya Tana River, Hussein Dado ametetea maendeleo yaliyopatikana chini ya uongozi wake huku akihimiza wakaazi wa Kaunti hiyoA� kuwakataa viongozi ambao wanahujumu mipango yake kabla ya uchaguzi mkuu wa mwezi Augosti. Gavana huyo ambaye anatetea kiti chake kwa tiketi ya chama cha Jubilee, alikuwa akihutubu wakati wa kampeini zake katika maeneo ya Hewani, na Wema. Dado alihimiza wakaazi hao kumchagua kwa muhula wa piliA� ili aweze kukamilisha miradi ambayo tayari imeanzishwaA� tangu alipoingia ofisini mwaka 2013. Akihutubia wakazi wa eneo la Hewani, Dado alisema iwapo atachaguliwa kwa muhula wa pili atasajili wazee elfu-40 chini ya mpango wa bima ya kitaifa ya matibabu (NHIF), hivyo kuwawezesha kupata huduma bora za matibabu. Gavana huyo anakabiliwa na upinzani kutoka kwa Danson Mungatana wa chama cha KPP; na pia Meja mstaafu Dhadho Godhana wa chama cha ODM; miongoni mwa wawaniaji wengijne wa kiti hicho cha Ugavana.