Gavana Atoa Senti Zake Mbili Kuhusu Wabunge Waasi

Gavana wa Machakos, Alfred Mutua amekashifu hatua ya chama cha Wiper ya kuwaondoa wabunge Regina Ndambuki, John Munuve na Joe Mutambu kwenye kamati za bunge. Mutua amesema hatua hiyo inahujumu demokrasia. Alisema wabunge hao watatu wameadhibiwa kwa kujihusisha na siasa za maendeleo. Wabunge hao waliondolewa kwenye kamati hizo za bunge kama hatua ya kuwaadhibu kwa kuasi msimamo wa chama cha Wiper katika maswala ya bunge.