Gavana Ali Hassan Joho aapishwa kwa kipindi cha pili

Gavana wa kaunti ya Mombasa, Hassan Joho, aliapishwa jana kwa kipindi chake cha pili na cha mwishoA� kwenye sherehe iliyohudhuriwa na vinara wa muungano wa NASA , Raila Odinga na Musalia Mudavadi. Akiongea wakati wa sherehe hiyo ya kuapishwa iliyoandaliwa katika bustani ya Mama Ngina, Joho alikariri kujitolea kwake kuwahudumia wakazi wa Mombasa. Aliahidi kutoa nafasi zaidi za kazi kwa vijana, kuimarisha usalama na kuimarisha uchumi wa kaunti hiyo ambayo uchumi wake unategemea sana utalii na bandari ya Mombasa. Joho pia alitangaza azma yake ya kuwania Urais wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2022. Kwa upande wake , Raila alimpongeza JohoA� kwa kuchaguliwa tena gavana wa kaunti ya Mombasa na akawashukuru watu wa Mombasa kwa kumpigia kura kwa wingi wakati wa uchaguzi mkuu wa hivi majuzi.