Garissa yakumbwa na mafuriko

Wakulima ambao hutumia mbinu ya kunyunyizia mashamba maji hukoA� Sankuri, kaunti ya Garissa wamepata hasara kubwa baada ya mimea yao kuharibiwa wakati wa mvua kubwa iliyosababisha mashamba yao kufurika. Uchunguzi uliofanywa na shirika la habari la KNA katika baadhi ya mashamba huko Sankuri na Hadley ulibaini kuwa wakulima hao hawawezi kufika kwenye mashamba yao yaliofurika na sasa huenda wakapata hasara ya mamilioni ya pesa.Baadhi ya mazao yalikuwa tayari kuvunwa zikiwemo nyanya na aina mbali mbali ya mboga.Mvua kubwa iliyoanza kunyesha katika sehemu kadha za kaunti ya Garissa,pamoja na kaunti jirani zaA� Tana River na Kitui imesababisha mafuriko makubwa na kuufanya mto Tana kuvunja kingo zake.Mgombeaji wa kiti cha ubunge cha Balambala Abdi Omar Shurie alizuru sehemu hiyo na kuitaka idara ya kukabiliana na mikasa kuwasaidia wakulima hao.Siku ya jumamosi helikopta ya kijeshi iliokoa familia ya watu 14 kutoka kwenye mafuriko katika sehemu ya Hadley tarafa ya Sankuri.