Maafisa 5 Wa Polisi Wauawa Katika Shambulizi La Kigaidi Mandera

Maafisa watano wa polisi waliuawa leo asubuhi wakati gari lao liliposhambuliwa na washukiwa wa kundi la Al Shabaab huko Mandera. Polisi wamesema gari hilo lilishambuliwa kwaA�guruneti katika eneo la Dabacity karibu na Elwak. Gavana wa Mandera, Ali Roba aliyethibitisha kisa hicho alishtumu shambulizi hilo huku akiwakashifu maafisa wa polisi kwa kutochukua hatua licha ya kupokea taarifa za kijasusi. Shambulizi hilo limejiri siku moja baada ya kundi hilo la kigaidi kuthibitisha kwamba mshukiwa wa shambulizi la chuo kikuu cha Garissa, Wali Kuno Dulyadeen kwa jina lingine Gamadheere, aliuawa hivi majuzi katika shambulizi la ndege nchini Somalia.