Gari La Kampuni Ya Teksi Ya Uber Lateketezwa

Gari moja la teksi la kampuni ya Uber liliteketezwa jana usiku na dereva wake kujeruhiwaA� baada ya kushambuliwa na wahalifu kutokana na ushindani wa kibiashara mjini Nairobi.Dereva huyo alikuwa amemfikisha mteja nyumbani kwakeA� kwenye barabara ya KirichwaA� jana usiku aliposhambuliwaA� baada ya gari lake kufungiwa na jingine.Akithibitisha kisa hicho OCPDA� wa kituo cha KilimaniA� Peter Kattam alisema kuwa uchunguzi umeanzishwa kuhusiana na kisa hicho.Akizungumza na KBC kwa njia ya simu Kattam alisema kuwa gari hilo lilikuwa limeshamfikisha mteja kwake mwendo wa saa tatu usiku kisa hicho kilipotokea.Kisa hicho kimetokea baada ya vingine kadhaa ambapo wahudumu wa taxi wamekuwa wakishutumuA� taxi za kampuni hiyo kwa kutotoa huduma kwa kuzingatia sheria za taxi za kampuni nyinginezo za humu nchini.Madereva wa texi za Uber wameshutumiwa kwa kutoza nauli ya chini kuliko wenzao na hivyo kuwapokonya biashara.