Gareth Bale hatashiriki katika mechi dhidi ya Uhispania

Kocha mkuu wa timu ya soka ya Wales  Ryan Giggs  ametangaza kuwa mchezaji  Gareth Bale hatashiriki katika mechi ya leo dhidi ya Uhispania na pia mechi ya ligi ya mataifa dhidi ya Jamhuri ya Ireland Jumanne ijayo.

Bale hakufanya mazoezi kwa mara ya tatu  mfululizo jana  baada ya kujeruhiwa kiuno wakati Real Madrid  ilipoishinda Alaves bao 1-0  katika mechi ya  La Liga mwishoni mwa juma lililopita alipobadilishwa dakika 10 kabla ya kipenga cha mwisho kupulizwa.