Fred Ouda aibuka mshindi

Mwakilishi wa wadi ya Gem Fred Ouda ameshinda uchaguzi wa mchujo wa A�ODM uliorejelewa ili kumteua mgombeaji wa kiti cha eneo bunge la Kisumu Central kwa tikiti ya chama hicho kwenye uchaguzi mkuu ujao.Wakati wa uchaguzi huo wa mchujo uliorejelewa jana,Ouda alipata kura 6,694 akifuatiwa na aliyekuwa katibu mkuu wa chama cha TNA ambaye alihamia chama cha ODM mwezi Jaruary,Onyango Oloo ambaye alijipatia kura 4,991.Mbunge wa sasa wa eneo bunge hilo Ken Obura alikuwa wa tatu kwa kura 1,040. Ouda alitangazwa mshindi na afisa aliyesimamia uchaguzi huo Samson Odoyo McOremo ambaye alisema matokeo hayo ni ya kutoka vituo 36 vya kupigia kura kati ya 45.Alisema matokeo kutoka vituo tisa vilivyosalia vya kupigia kura hayakujumuishwa miongoni mwa matokeo ya mwisho ya kujumuishwa kwa kura kwasababu maafisa waliosimamia uchaguzi katika vituo hivyo waliyaacha masanduku ya kura katika kituo cha kujumuisha hesabu za kura na kutoweka.Awali taharuki ilitanda katika taasisi ya Goan Institute, ilyoko eneo bunge la Kisumu Central ambako kura zilijumuishwa kwa madai kwamba badhi ya masanduku hayakuwasilishwa.Polisi walilazimika kutumia vitoza machozi kuwatawanya watu waliokuwa wamekusanyika nje ya kituo hicho.