Fred Matiang’i Atarajiwa Kutoa Ripoti Kuhusu Mikasa Ya Moto Shuleni Mwisho Wa Juma Hili.

Wizara ya elimu imesema ripoti kuhusu mikasa ya moto shuleni itatolewa mwishoni mwa juma hili. Akiongea kwenye taasisi ya mafunzo ya uongozi nchini waziri wa elimu Fred Matianga��i alitoa wito kwa maafisa wa vyama vya walimu kusaidia katika utekelezaji wa ripoti hiyo itakapokamilika. Alisema ombi hilo linatokana na ukweli kwamba mara nyingi vyama vya walimu vimekuwa kikwazo kwa baadhi ya mabadiliko ambayo wizara hiyo inatekeleza shuleni.
Alisema migawanyiko katika sekta ya elimu inakwamisha marekebisho yanayonuiwa kuwanufaisha wanafunzi. Kumekuwa na visa kadhaa vya migomo shuleni huku shule ya upili ya wavulana ya St. Petera��s kwenye eneo la Kandara kaunti ya Muranga��a ikiwa ya hivi punde zaidi kufungwa kwa muda usiojulikana. Hii ni baada ya bweni kuteketea juma hili ambapo wanafunzi 123 waliachwa bila malazi. Wanafunzi tisa wa kidato cha nne wanazuiliwa na maafisa wa polisi huku uchunguzi ukiendelea.