Fred Gumo Ampigia Upatu Eugene Wamalwa Kuwania Ugavana Kaunti Ya Nairobi

Aliyekuwa mbunge wa Westlands Fred Gumo amempigia upatu waziri wa maji Eugene Wamalwa kuwania ugavana kaunti ya Nairobi. Mwanasiasa huyo mkongwe anaamini kuwa Wamalwa ana maarifa na ujuzi wa kisiasa wa kusimamia masuala ya jiji la Nairobi. Hata hivyo hakuchelea kupuuzilia mbali madai kwamba wamalwa analazimishiwa wakazi wa jiji na rais na naibu wake. Kujiunga kwa Wamalwa kwenye kinyanganyiro cha kuwania ugavana wa Nairobi kunazua kizungumkuti kwa siasa za Jubilee kwani wengine katika muungano huo kama vile seneta wa Nairobi Mike Sonko, mbunge wa dagoretti kusini Dennis Waweru, aliyekuwa mbunge wa Starehe askofu Margaret Wanjiru na mwenyekiti wa chama cha TNA Johnson Sakaja pia wameeleza azma yao ya kuwania kiti hicho. Letu sasa ni kusubiri kuona ni nani atakayewania kiti hicho cha ugavana kwa tiketi ya chama cha Jubilee