Frank Nuttal Kutia Saini na Kilabu Ya Zamalek Ya Misiri

Kocha mkuu wa timu ya Gor Mahia, Frank Nuttal anatarajiwa kutia saini mkataba leo na kilabu cha Zamalek kinachoshiriki katika ligi kuu ya soka nchini Misri. Baada ya kuiongoza Gor Mahia kwa muda wa miezi 18, Nuttal mzaliwa wa Skotland, ameamua kujiunga na timu ya Zamalek kuwa msaidizi wa aliyekuwa mkufunzi wa Aston Villa; Alex McLeish.

Nuttal aliwasili jijini Kairo jana usiku na alitarajiwa kuhudhuria mazoezi ya kilabu hicho kinachojiandaa kucheza na timu ya a�?Uniona�? inayoshiriki katika ligi kuu ya soka nchini Kameruni, katika mechi ya kuwania kombe la taifa bingwa barani Afrika mwishoni mwa juma hili.

Alijiunga na Gor Mahia mwezi September mwaka 2014, alipotia saini mkataba wa miaka mitatu kisha akaongeza muda hadi mwaka 2015.

Aidha, Nuttal aliisaidia timu hiyoA� kunyakua taji nne: Taji ya kombe la DStv, taji mbili za ligiA� kuu na moja ya timu nane bora. Hali kadhalika aliiongoza Gor Mahia kufuzu kwa fainali ya kombe la CECAFA Kagame, ambapo ilishindwa na wenyeji Azam mabao mawili kwa bila, jijini Dar Es Salamm.

Nuttal ataiaga Gor Mahia baada ya kupoteza mechi nane muhimu; mbili dhidi ya AC Leopards kutoka Kongo, moja dhidi ya Azam na nyingine dhidi ya timu ya Nakumatt katika nusu fainaliA� ngao ya GOtv; mwaka jana. Kuanzia mwanzo wa mwaka huu; Nuttal amepoteza mechi nne peke; mbili dhidi ya CNaPS ya Madagaska, dhidi ya Bandari na nyingine ya ligi dhidi ya AFC Leopards juzi.