Francis Nyenze azikwa leo

Aliyekuwa mbunge wa Kitui Magharibi, Francis Nyenze anazikwa leo katika eneo la Kabati, kaunti ya Kitui. Miongoni mwa wanaohudhuria mazishi hayo ni naibu wa rais William Ruto na kiongozi wa muungano wa NASA Raila Odinga. Nyenze alifariki tarehe 6 mwezi huu alipokuwa akipokea matibabu katika hospitali ya Nairobi. Marehemu Nyenze amekuwa akiuguza maradhi ya saratani ya utumbo kwa miaka 10. Nyenze alizaliwa tarehe 2 mwezi Juni 1957 katika eneo la Kabati, Kitui Magharibi. Uzito wa maradhi yaliyomkumba ulithihirika wakati aliposhiriki sherehe ya kuapishwa kwa wabunge akiwa amebeba mtungi wa hewa ya oxygen. Nyenze ambaye alikuwa mwanachama wa chama cha Wiper alizua kiwewe wakati yeye na aliyekuwa mwenyekiti wa kitaifa wa chama hicho David Musila walipomuunga mkono rais Uhuru Kenyatta wakati wa uchaguzi mkuu wa mwezi Agosti. Nyenze aliwahi kuhudumu kama waziri wa mzingira mnamo mwaka 1997. Amemwacha mjane na watoto watatu.