Francis Atwoli akashifu vikali hatua ya Henry Rotich

A�Katibu mkuu wa shirikisho la vyama vya wafanyikazi-COTU, Francis Atwoli amekashifu vikali hatua ya waziri wa fedha, Henry Rotich ya kuzindua ushuru wa thamani wa ziada wa asilimia-16 kutozwa bidhaa za mafuta. Kwenye taarifa, Atwoli amesema waziri Rotich anapaswa kubuni mbinu mbadala za kukusanya mapato badala ya kuzindua ushuru dhidi ya bidhaa za mafuta. Alidai kuwa Rotich na tume ya kudhibiti sekta ya kawi wamepuuza wito wa wananchi wa kawaida wa kwa kutoza ushuru bidhaa za mafuta. Alihimiza serikali kuondolea mbali ushuru huo. Atwoli alisema ushuru huo utawatoa motisha wawekezaji na kusabbaisha uhaba wa ajira. Shirikisho la COTU limeitaka tume ya ERC kupunguza bei ya bidhaa za mafuta na kawi.