Florentin Pogba asema yuko tayari kukabiliana na Paul kuwania kombe la kilabu bingwa

Ndugu wa Paul Pogba, Florentin Pogba, amesema kuwa yuko tayari kukabiliana na nyota huyo wa Manchester United ili kuisaidia timu yake St Etienne kutwaa ushindi timu hizo zitakapomenyana Alhamisi hii kuwania kombe la kilabu bingwa Ulaya. Florentin Pogba, atakabiliana na Paul kwa mara ya kwanza tangu walipokuwa wakicheza pamoja utotoni nchini Ufaransa walikolelewa. Florentin amesema amejiandaa kumenyana na Paul Pogba ambaye ni mchezaji aliyenunuliwa ghali zaidi kuliko mchezaji mwengene yeyote Barani Ulaya watakapopimana nguvu uwanjani Old Traford. Ndugu hao wawili watakuwa wa kwanza kukabiliana uwanjani baada ya Rio na Anton Ferdinand kufanya hivyo. Wakati uo huo, mechi 16 zimeratibiwa kuchezwa siku iyo hiyo, ambapo Celta Vigo itamaliza udhia na Shaktar Donetsk nayo Villarreal ipimane nguvu na Roma.