Florence Kiplagat atwaa ubingwa kwa mara ya nne katika nusu marathoni

Florence Kiplagat alitwaa ubingwa katika mbio za nusu marathoni za Baselona kwa mara ya nne mfululizo, kwa muda wa saa moja dakika nane sekunde 15 jana usiku, nchini Uhispania. Kiplagat alitarajiwa kuvunja rekodi mpyaA�A�ya Peres Jepchirchir aliyoiandikishaA�A�Ijumaa iliyopita katika mbio za marathoni za RAK, katika Milki za Kiarabu. Hata hivyo, Kiplagat alichelewa kwa muda wa dakika mbili. Katika kitengo cha wanaume mshindi alikuwa Leonard Kipkoech Langa��at aliyewaongoza Wakenya kumaliza katika nafasi za nne za mwanzo katika muda wa saa moja sekunde 52. Meschack Koech alimaliza katika nafasi ya pili kwa muda wa saa moja sekunde 54 huku Joel Kimurere akiridhika na nafasi ya tatu kwa muda wa saa moja sekunde 59. Mshindi mara mbili duniani Abel Kirui alimaliza wa nne