Finali za CHAN kuchezwa kesho

A�Mechi za nusu fainali ya kuwania kombe la Bara Afrika kwa wachezaji wa ligi za nyumbani CHAN zitachezwa kesho huku wenyeji Morocco wakichuana na Libya katika mechi ya kwanza.Morocco ilifuzu kwa nusu fainali baada ya kuipiku Namibia mabao mawili kwa sifuri jijini Casablanca siku ya Jumamosi.Ayoub El Kaabi, alifunga bao lake la sita mchuanoni na kuipa Morocco uongozi kisha Salaheddine Saidi akaongezea bao la pili dakika kumi baada ya kuanza kwa kipindi cha pili. Libya kwa upande mwingine ilifuzu baada ya kuilaza Jamhuri ya Congo mabao matano kwa matatu kwa njia ya penalti. Nusu fainali ya pili itakuwa baina ya Sudan na Nigeria. Sudan ilifuzu ilipoishinda Zambia bao moja kwa sifuri nayo Nigeria ikailaza Angola mabao mawili kwa moja.