FA yatoa sheria mpya kwa wachezaji wanaojiangusha uwanjani

Wachezaji watakaojiangusha uwanjani kwa nia ya kuwalaghai marefa wa michuano ya soka nchini Uingereza watapigwa marufuku kuanzia msimu ujao, kulingana na sheria mpya za chama cha FA.A� Chini ya sheria hizo mpya zilizopitishwa na chama hicho katika mkutano wao wa kila mwaka hapo jana, jopo litatazama kanda za video za michuano yote ya mwishoni mwa juma siku ya Jumatatu likitafuta kesi za wachezaji wanaojiangusha kuwalaghai marefa. Aidha mchezaji yeyote atakayepatikana na hatia ya kujiangusha uwanjani atapigwa marufuku. Chama cha FA pia kimesema kuwa kimepitisha marekebisho yaliyopendekezwa mwezi Machi, baada ya kulaumiwa zaidi kwa jinsi kinavyoendeshwa.