Ezekiel Mutua Asisitiza Haja Ya Matumizi Ya Mitandao Ya Kijamii Kuimarisha Amani Nchini

Afisa mkuu wa bodi ya kuorodhesha filamu nchini Ezekiel Mutua amesisitiza haja ya matumizi ya vitandazi vya kijamii kuimarisha maadili bora na amani hapa nchini. Mutua alisema huku kukiwa na manufaa ya kiuchumi na kijamii pamoja na manufaa mengine mengi, pia kuna hatari zinazotokana na vitandazi hivyo kama uhalifu kupitia mtandao . Mutua aliyekuwa akiongea katika hoteli moja mjini Mombasa baada ya kongamano la kila mwaka la usalama na teknologia ya habari hapa nchini , alisema kuwa bodi hiyo inaangazia upya mswada wa filamu kuufanyia marekebisho ya kujumuisha vyombo vya habari kupitia mtandao na usambazaji wa filamu. Aliangazia ufanisi wa teknolojia ya habari kwa jamii ikiwa ni pamoja na huduma za kutuma pesa kupitia simu za rununu lakini akawaonya wananchi dhidi ya matumizi mabaya ya vitandazi hivyo vya kijamii.