Wamalwa Asema Wizara Yake Imezindua Mpango Wa Kuimarisha Hifadhi Za Maji Kote Nchini

Waziri wa maji, Eugene Wamalwa amesema wizara hiyo imezindua mpango mahsusi wa kuimarisha hifadhi ya maji katika kaunti zote hapa nchini akisema kuwa serikali imetumia zaidi ya shilingi bilioni-10 kuhakikisha wakenya wanapata huduma za maji. Akiongea jana katika kanisa la mtakatifuA�Petro na Paulo katika kaunti ya Kiambu, Wamalwa alisema serikali imejitolea kusambaza huduma za maji kwa wakenya wote kwa kujenga mabwawa zaidi.

Mbunge wa Kiambu Mjini, Jude Njomo alisema asilimia-15 ya wakazi wa eneo hilo wana maji ya mfereji na kupongeza serikali ya Jubilee kwa kutenga zaidi ya shilingi miloni-20 kufadhili usambazaji maji ya mfereji katika eneo hilo. Wamalwa alisema wanashirikiana na serikali za Ufaransa na China kujenga vituo vya kuhifadhia maji katika kaunti ya Kiambu.