Esse Akida Awapiku Miamba Wa Soka Nchini Ureno CF Benfica Mabao Matatu Kwa Sufuri.

Esse Akida alifunga mabao matatu na kuisaidia timu ya taifa ya soka kwa akinadada, Harambee Starlets, kuwapiku miamba wa soka nchini Ureno CF Benfica mabao matatu kwa sifuri. Mechi hiyo ilikuwa ya ufunguzi wa makala ya tano ya kuwania kombe la COTIF kwa akinadada na ilichezwa jijini Valencia Uhispania jana usiku. Kiungo huyo mwenye makao yake jijini Mombasa, AkidaA� aliipa Starlets uongozi katika dakika ya thelathini. Katika kipindi cha pili binti huyo aliongeza bao la pili kisha akafunga la tatu dakika kumi kabla ya mechi kukamilika. Starlets itakabiliana na RDC Espanyol katika mechi yake ya pili ya michuano hiyo kesho. Timu sita zinashiriki katika kipute hicho zikiwamo: timu ya akinadada ya Venezuela, FC Benfica, RCD Espanyol na A�Real Betis ya Uhispania miongoni mwa nyingine. Kenya inatumia mashindano hayo kujiandaa kwa michuano ya kombe la Bara Afrika kwa akinadada mwezi Novemba mwaka huu nchini Kameruni.