Emmerson atafuta jinsi ya kuboresha uhusiano wao na mataifa ya Magharibi

Rais mpya wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa anatafuta kuondolewa kwa vikwazo vya mataifa ya Magharibi dhidi ya taifa hilo akisema vimelemaza ustawi wa kitaifa. Aidha amesema uchaguzi ambao umeratibiwa kufanyika Julai mwaka ujao huenda ukaandaliwa mapema. Akihutubia viongozi wa chama tawala cha Zanu PF Rais Mnangagwa alisema serkali itafanya kila juhudi kuhakikisha uchaguzi huo ni huru na wa haki.Rais Mnangagwa alichukuwa hatamu za uongozi mwezi jana baada ya aliyekuwa kiongozi wa muda mrefu wa taifa hilo Robert Mugabe kuondolewa mamlakani. Rais huyo anatarajiwa kuidhinishwa leo kuwa kiongozi wa chama cha ZANU-PF na pia mwaniaji wa chama hicho katika uchaguzi mkuu ujao. Mugabe mwenye umri wa miaka 93 na ambaye aliongoza taifa hilo kwa miaka 37, hajawahi kuonekana hadharani tangu kuondoka mamlakani. Hata hivyo aliyekuwa msemaji wake George Charamba alisema kuwa alikuwa amepelekwa nchini Singapore kwa uchunguzi wa matibabu.