Emmanuel Macron anyakua kiti cha urais Ufaransa

Mwaniaji wa urais wa siasa za mrengo wa kati nchini Ufaransa Emmanuel Macron ameshinda uchaguzi wa urais, dhidi ya mpinzani wake Marine Le Pen. Macron, mwenye umri wa miaka 39A�A�alipata aslimia 66.06 ya kura huku mpinzani wake akipata aslimia 33.94 ya kura na kuibuka rais wa kwanza chipukizi kuwahi kutawala taifa hilo. Aidha atakuwa rais wa kwanza kutoka chama kidogo wala sio viwili vikubwaA�A�jinsi imekuwa desturi tangu kuasisiwa kwa jamhuri mpya ya Ufaransa mwaka wa 1958.

Macron alisema taifa hilo limefungua ukurasa mpya katika historia yake na kwamba amesikia kilio na wasi-wasi wa raia. AliapaA�A�kuzipa umbele changamoto zinazolikabili taifa ambalo zinatishia umoja wa taifa hilo. Maelfu ya wafwasi wa Macron walimiminika nje ya jumba la ukumbusho wa mambo ya kale la Louve,katikati ya jiji la Paris, ambapo rais wao mteule alijumuika nao. Alisisitiza kuwa jukumu linalomkabili ni kubwa.