Jaji mkuu aondoa Ekuru Aukot kwenye marudio ya uchaguzi wa urais

Jaji mkuu ameondoa kwenye mahakama ya juu ombi la mgombeaji Urais wa chama cha Third Way Alliance, Dr. Ekuru Aukot la kutaka jina lake kuorodheshwe miongoni mwa wagombeaji Urais kwenye marudio yajayo ya uchaguzi wa Urais. Jaji mkuu David Maraga kwenye uamuzi wake alisemaA� mahakama ya juu haina uwezo wa kushughulikia masuala yaliyo kwenye ombi hilo na badala yake akamwelekeza mlalamishi katika mahakama kuu ili iamue iwapo atahusishwa kwenye marudio hayo ya uchaguzi wa Urais au la. Akiongea na wanahabari muda mfupi baada ya uamuzi huo kutolewa, Dr Aukot alisema atawasilisha ombi lake katika mahakama kuu kesho. Pia alisema kwamba kwenye ombi lake, ataiomba mahakama kuu kufutilia mbali arifa iliyochapishwa na tume ya IEBC kwenye gazeti rasmi la serikali kuhusiana na marudio ya uchaguzi wa UraisA� hadi pale ombi lake litakaposikizwa na kuamuliwa. Dr Aukot ambaye anataka aorodheshwe miongoni mwa wagombeaji Urais kwenye marudio ya uchaguzi huo, anasisitiza kwamba ni haki yake ya kidemokrasia kushiriki kwenye marudio ya uchaguzi huo na kutoorodheshwa kwake kunakiuka haki yake na ya wafuasi wake. Dr Aukot alisema tume hiyo ingeweza tu kutomuorodhesha kwenye uchaguziA� huo endapo mahakama ingeamuru uchaguzi huo uingie duru ya pili. IEBC inasisitiza kwamba uamuzi wake kuhusu watakaoshiriki kwenye marudio hayo ya uchaguzi wa Urais ulizingatia uamuzi wa mahakama ya juu wa mwaka 2013.