Edmond Salasia

Edmond Salasia ni mtangazaji aliyebobea na hukuletea kipindi cha Tafrija ya Taifa kila siku ya Jumatatu hadi Ijumaa kuanzia saa kumi hadi saa mbili usiku.


Amesomea stashahada ya utangazi kutoka chuo cha utangazaji cha KIMC. Alijijunga na shirika la utangazaji la KBC mwaka wa 2008.


Edmond amewahi kufanya vipindi vingine katika idhaa hii kama vile 'Pepea Afrika'. Licha ya kushamiri katika sekta ya utangazaji, amewahi vile vile kujihusisha na biashara katika soko la hisa.


Kando na utangazaji, anapenda kusafiri, kukwea milima, kutazama filamu, kuogelea na hata kucheza mchezo wa gofu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *