Eden Hazard asema haogopi kuchuana na Paris St German au Baselona

Kimataifa, kiungo wa timu ya Chelsea inayoshiriki katika ligi kuu ya soka nchini Uingereza, Eden Hazard, amesema timu hiyo haiogopi kuchuana na Paris St Germain au Baselona katika mechi za timu 16 bora za kombe la kilabu bingwa Barani Ulaya.Hii ni baada ya Chelsea kutoka sare na Atletico Madrid, bao moja kwa moja, jana usiku, uwanjani Stamford Bridge huku Chelsea ilikosa nafasi ya kuliongoza kundi lao. Atletico Madrid iliongoza katika kipindi cha kwanza kupitia kwa Saul Niguez lakini Chelsea ikasawazisha baada ya Stefan Savic kujifunga kipindi cha pili. Katika matokeo ya mechi nyingine; Baselona iliipiku Sporting Lisbon mabao mawili kwa sifuri, Bayern Munich ikailaza PSG mabao matatu kwa moja nayo Manchester United ikaishinda CSKA Moscow mabao mawili kwa moja. Juventus iliishinda Olympiacos mabao mawili kwa sifuri. Aidha, Mechi nane zitachezwa leo usiku ikiwamo ole baina ya mabingwa watetezi Real Madrid dhidi ya Borussia Dortmund.